Bondia mtanzania Abdallah Pazi ambaye maarufu kwa jina la Dullah Mbabe amefunguka katika exclusive interview kuhusiana na ushindi wake wa Ubingwa wa Dunia wa WBO Asia Pasific uzito wa kati kwa kumpiga bondia Zulipikaer Maimaitiali wa China kwa KO (Knock Out) round ya 3.

Pambano hilo lilifanyika Qing Dao nchini China, Zulipikaer ndio bondia namba moja China ambapo alivuliwa mkanda huo baada ya kupigwa na Dullah Mbabe,  tukio ambao lilimfanya Dullah mbabe kuchukua headlines sana.

AyoTV imempata Dullah Mbabe na kumuuliza maswali kadhaa kuhusiana na pambano na ushindi huo lakini kubwa kwani nini aliondoka kimya kimya? pili ametumia mbinu gani kushinda kwani mabondia wengi wa Tanzania wakienda nje wanalalamikia hujuma, Dullah amesema mbinu pekee ya kushinda ugenini ni kuhakikisha unampiga mpinzani wako KO.