Ronaldo, amwaga machozi baada ya kuulizwa sawali kuhusu baba yake, Alipoulizwa jinsi alivyokuwa akijisikia baada ya  kusikia baba yake akiongea juu ya kiburi chake kwa mafanikio ya mwanawe, mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid aliongezea:“Ndio.”Nadhani mahojiano yangekuwa ya kuchekesha, lakini sikutarajia kama ntalia kulia. Lakini sikuwahi kuona picha hizi wala “Sijawahi kuona video yeyote kitu ambacho hakiwezekani” Sijui iko wapi … Lazima niwe na picha hizo kuonyesha familia yangu. “Lakini sikumjua baba yangu asilimia 100. Alikuwa mtu mlevi sana. Sikuwahi kuongea naye, kama mazungumzo ya kawaida. Ilikuwa ngumu sana ”

Ronaldo aliongeza kuwa “Familia yangu imeona mafanikio yangu, mama yangu ameyaona, Ndugu zangu pia, hata mtoto wangu wa kwanza pia, lakini baba yangu, hakuona chochote, pia hakuona wakati nashinda tuzo na ilitakiwa ayaone… alikufa angali mdogo. ”