Serikali ya Tanzania imesitisha safari zake za ndege kwenda nchini Afrika Kusini kutokana na vurugu zinazoendelea nchini humo.

Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amesema watasitisha kwa muda safari hizo mpaka pale serikali ya Afrika Kusini itakapowapa thibitisha kwa maandishi juu ya usalama wa abiria na chombo vyombo vya usafiri.