Mahakama Kuu ya jimbo la Gauteng imeamuru ndege ya Air Tanzania iliyokuwa ikishikiliwa nchini Afrika Kusini kuachiwa mara moja.

Mwandishi wetu wa Afrika Kusini Nomsa Maseko anasema kuwa michakato ya kuichilia ndege hiyo kurejuea Dar es Salaam ikitokea katika uwanja wa ndege wa OR Tambo jijini Johannesburg inaendelea.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Dkt Damas Ndumbaro aliyekuwepo mahakamani ameileza BBC kuwa Tanzaia imeridhishwa na uamuzi wa mahakama.

Mkulima ambaye alipeleka shauri hilo mahakamani Hermanus Steyn na kupata kibali cha kushikiliwa ndege hiyo, Hermanus Steyn hajaridhishwa na hukumu.

Mwandishi wa BBC Maseko anaripoti kuwa Bw Steyn amekata rufaa, na shauri hilo linatarajiwa kuanza kusikilizwa leo hii.