Muigizaji na mchekeshaji  Idris Sultan, amepiga stori na EATV & EA Radio Digital, kuhusu suala la utani wake kwa rapa Billnass na kutaka kupigwa na msanii wa filamu Ray.


"Unajua ni kijana ambaye anaidhalilisha Kinondoni, na ndiyo mkazi mkubwa sana wa Kinondoni, namuangaliaga tu siwezi kuongea sana maana ni mtu wa kulialia sana, huwa napigiwa na familia yake kuulizwa kuwa nimemfanya nini Billnass mbona analia ameshindwa kulipia kodi, nikawajibu hata akiwaga halii mbona hawezi kulipa kodi" Idris Sultan akimzungumzia Billnass.

Idris Sultan ameeleza mkasa aliokutana nao baada kumtania msanii wa filamu Vincent Kigosi 'Ray' kwa kusema watu huwa wanachukiaga kiukweli ila kuna muda huwaga wanaelewa lakini hawezi kukwambia kama amekasirikia nini au watu wanaingiziaga vya kwao kwamba wanani-mind.

Pia ameendelea kusema kuna siku alikutana na Ray maeneo ya viwanja vya 'Leaders' kipindi alivyokuwa anataniwa suala la maji, ambapo alivutwa pembeni akaambiwa achague kati ya kupigwa ngumi au kichwa ila alikimbia na hajaonana na msanii huyo hadi leo.