MKUU wa Wilaya ya Iringa, Dkt. Richard Kasesela amewaomba radhi familia na Watanzania wote kuhusu taarifa aliyoitoa kuwa aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania (Aprili 24, 1984 – Novemba 5, 1985), Dkt. Salim Ahmed Salim amefariki dunia.Amesema taarifa hizo si za kweli, amefuatilia na kujiridhisha kuwa Dkt. Salim huyo yupo hai  anaendelea na matibabu yake nchini Uingereza.


“Apologize for the wrong msg Dr Salim anaendelea vizuri I have re checked again.”“I highly apologize Dr Salim Ahmed Salim is still alive anaendelea na Matibabu Uingereza nimeongea na familia. It’s unfortunate the source of the earlier msg was wrong. I highly apologize kwa familia na Watanzania kwa ujumla.”