MWANAMUZIKI na mwandaaji wa muziki nchini Tanzania, Quick Rocka,  leo amepiga stori na kipindi cha BONGO 255 ndani ya studio za +255Global Radio akifunguka mengi kuhusu muziki wake na mahusiano yake.Alisema pamoja na kuonekana kushiriki tamthilia  na akiwa amepotea kidogo katika muziki,  amesema hawezi kuacha muziki  kwani anahueshimu sana na umemfunghulia milango mingi.

Pia amefunguka kwamba mbali na muziki yeye pia ni dalali wa magari  na vipuri vyake.Kuhusu mahusiano yake na  mrembo kutoka Uganda, Zari The Boss Lady ambapo wameonekana wakiwa pamoja na kuzua gumzo mitandaoni, Rocka amesema “uhusiano wangu na Zari umeanza kutokana na kazi tunayofanya.” alisema.