MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mrundi Amissi Tambwe ameonyesha kusikitishwa na kitendo cha straika wa Simba, Adam Salamba kuomba msamaha baada ya kuonekana akimwomba njumu staa wa Sevilla, Ever Banega, Alhamisi iliyopita.Salamba alifanya hivyo baada ya kumalizika kwa mchezo wa kirafiki ambao Simba ilipambana na Sevilla inayoshiriki La Liga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kufungwa mabao 5-4.


Akizungumza na Spoti Xtra, Tambwe alisema kuwa; “Kwa hiyo binafsi sikuona sababu ya Salamba kuomba samahani juu ya hilo, lakini inawezakana kwake yeye aliona ni kosa amefanya.”“Ila ningekuwa mimi wala nisingeomba msamaha kwa sababu hilo siyo kosa hata Ulaya wachezaji wengi tunaona kila siku wanafanya hivyo na hakuna anayeomba msamaha kwa sababu wanajua nini maana ya Fair Play,” alisema Tambwe ambaye bado hajajua hatma yake ndani ya Yanga.