MCHEZO wa mwisho kesho wa ligi kuu kati ya Mtibwa Sugar na Simba utakaochezwa uwanja wa Jamhuri umebadilishwa muda kutoka saa 10:00 mpaka saa 9:00 alasiri.

Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa sababu kubwa ya mchezo huo kubdailihwa muda ni kutokana na uwepo wa sherehe ya kukabidhiwa ubingwa kwa Simba ambayo itafanyika kesho.

Kifaru amewaomba mashabiki na wadau wa Mtibwa kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kuwashangilia wachezaji wao.