Msanii wa muziki wa injili nchini, Joel Lwaga amesema hakuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii wa filamu Muna Love kama watu walivyokuwa wakizungumza kwenye mitandao.

Akipiga story na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Joel amesema kuwa hakuwahi kusema mbele ya umma kuwa ana uhusiano naye lakini walikuwa na ukaribu wa kawaida.

"Sikuwahi kuwa na uhusiano na Muna kwani kupitia lile pia limenipa nguvu na kuniimarisha, na halijanipa shida mimi sana sana limeniongezea mashabiki", amesema Joel.

"Mimi sina la kumwambia Muna zaidi ya kumwambia tu, afanye lolote linalompa furaha na amani mwenyewe na asikate tamaa matatizo ni sehemu yetu binadamu", ameongeza Joel.

Wawili hao waliingia katika mijadala mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii iliyodai kuwa walikuwa na uhusiano wa kimapenzi na walikuwa mbioni kufunga ndoa, baada ya kifo cha aliyekuwa mtoto wa Muna Love Patrick ambaye alifariki akiwa nchini Kenya alikokuwa akipatiwa matibabu na Joel pia alikuwepo huko.